Wedding Day: Mr. & Mrs. Christopher Mambo- Aloyson

By

on

Kampuni ya BONGOHOOD na mtandao huu wa ALOYSON.COM unakuletea matukio ya sherehe nzima ya Bw. na Bi. Christopher Mambo (watoto wa mzee Michael Mambo mmiliki wa shule ya kimataifa ya THEMI HILL) kwenye siku yao muhimu duniani.

Ndoa ilifungwa katika kanisa Katoriki la Familia Takatifu (Holly Family) la Parokia ya Ipuli- Tabora siku ya tarehe 03 Juni, 2017 mchana huku kwaya ya FAMILIA TAKATIFU ya Ipuli ikiongoza Liturujia, baadae wakachukua kumbukumbu chache za picha pale TABORA BELMONTE HOTEL na hatimaye jioni kujongea ukumbi wa MUUNGANO MESSY uliopambwa vizuri na MAMA CHIVINJA wa Tabora huku shughuli ikiongozwa na MC TIDOH wa Arusha.

KUMBUKA: Kumbukumbu zote za picha mwendo (video) na picha mnato ziliwekwa na kampuni la BONGOHOOD.

Sherehe ilibahatika kuhudhuriwa na kiongozi wa mkoa Ndg, Agrey Mwanri na mkuu wa wilaya Mwl Queen Mlozi wakifuatiwa na wafanyabiashara mashuhuri Tabora mjini.

Kanisa la RC Ipuli- Tabora

Bw. na Bi. Christopher

Bw. Harusi akisoma somo la kwanza

Viapo mbalimbali vikiendelea kanisani.

Christopher akimvisha pete Marietha kama ishara na utambulisho wa kuwa wameungana kiimani na kuwa mwili mmoja hadi kufa.

Marietha akimvisha pete mmewe

Bw. Thoy, mwl wa kwaya na mpiga kinanda wa kwaya ya Familia Takatifu ya parokia ya Ipuli

Bw. & Bi. Michael Mambo (wazazi wa bwana harusi)

Wazazi wa Marietha (Bibi harusi)

Utiaji wa saini katika vyeti vya ndoa

Familia zote zaungana katika picha ya pamoja

HAPA UNAPATA KUTIZAMA PICHA ZA UKUMBINI USIKU.

kushoto ni Sanya JR (M/Kiti wa kamati ya mafanikio) na kulia ni mzee Vimajo (Flow manager) wote wafanyabiashara mashuhuri mjini Tabora

KUTOKA KUSHOTO: Frado, Sanya JR, Vimajo na Big Sele

Squad ya waharusi ikitinga ukumbini

Sherehe ikifunguliwa rasmi pale Bw. na Bi Christopher wakikata utepe.

Ufunguzi wa sala katika sherehe ya Bw. na Bi Christopher ikiongozwa na mama Vimajo

Salamu za mkuu wa mkoa wa Tabora ndg, Aggrey Mwanri kwa Bw. na Bi Christopher na waalikwa wote ukumbini.

Mkuu wa mkoa aliwapongeza Bw. na Bi Christopher kwa maamuzi sahihi ya kuoana kiutaratibu akisisitiza vijana wengine kuiga mfano huo, kwa upande mwingine alipongeza jitihada za baba wa bwana harusi ndg, Michael Mambo kuwa ni miongoni mwa wananchi wanaosaidia kukuza elimu mkoani hapo kupitia shule yake ya ENGLISH MEDIAM inayofahamika kama “THEMI HILL” ikiwa ni moja ya sera yake mkuu wa mkoa ya kuhakikisha Tabora inakuwa na wahitimu wengi watakaofikia kiwango cha elimu ya juu.

Hakuishia hapo, alisisitiza zaidi suala alilolianzishwa la kuhakikisha Tabora inakuwa ya kijani kwa kuleta mpango mkakati wa upandaji na utunzaji miti.

Mshereheshaji TIDOH wa Arusha katika usiku wa Bw. na Bi Christopher

Utambulisho na uwasilishwaji wa zawadi za kamati ya mafanikio katika usiku wa Bw. na Bi Christopher

G. Mafole M/M/Kiti wa kamati ya mafanikio na mmiliki wa Gonala Phamacy akitoa uwasilisho wa zawadi za kamati ya sherehe ya Bw. na Bi Christopher

Mama Queen Mlozi (Mkuu wa wilaya ya Tabora) akishiriki zoezi la kufungua Champagne katika usiku wa Bw. na Bi Christopher

Meza ya wazazi wa Bi. Marietha

Ndafu, maarufu kama keki ya Wachaga

Wosia wa vitendo kutoka kwa Mc Tidoh uliowaacha waalikwa midomo wazi huku ujumbe ukiwafikia Bw. na Bi Christopher na wanandoa wengine na ambao hawajaingia kwenye maisha ya ndoa

Burudani iliyokonga nafsi za waalikwa wengi


Mtandao wa ALOYSON.COM ikishirikiana na BONGOHOOD wanakupa wasaha wa mteja wao kufanyiwa au kuchukuliwa kumbukumbu zote muhimu na mahususi kama harusi, send off, birthdays, anniversaries, graduation, biashara, matangazo na matukio mengineyo katika picha mnato na mwendo kwa bei ndogo sana.

WASILIANA NASI: PIGA +255 755 103 054 | INSTAGRAM: @aloysonjr | FACEBOOK: @aloysonjr | TWITTER: @aloysonjr | YOUTUBE: @aloysontv

Comments/ Maoni