General

Lapiano Pub (Shimoni) Yabomolewa; Yajengwa Upya [Picha]

By

on

LaPiano Pub (Shimoni) yabomolewa hovyohovyo, maboresho babu kubwa yanakuja, pata kutazama picha na ujue siri ya urembo ya eneo ambalo lilijivutia umaarufu mkubwa ghafla na watu baadhi maarufu kufanyia maonesho humo akiwemo Genevive anayetamba na kibao cha NANA huyu ni mwanadada aliyekuwa mrimbwende wa Tanzania 2010.

Makorokoro yakitolewa baada ya kuta za LaPiano maarufu kama Shimoni kuvunjwa

lilipokuwa shimo la LaPiano pub

Lilipokuwa shimo la LaPiano pub

Shughuli ya uondoaji wa mabaki ya kuta ikiendelea

Mabaki ya kuta

Mmiliki wa Lapiano pub maarufu kama shimoni Bw. Nico ameuambia mtandao wa aloyson.com kuwa ubomozi wa jengo lile la kizamani lililokuwa limejengwa kwa miti na tope sasa kuboreshwa zaidi, maboresho hayo yanafuatiwa baada ya changamoto za kiburudani kuwa kubwa mjini Tabora kutokidhi mahitaji ya wanaopenda burudani hasa ya kumbi za kuchezea mziki.

Ameahidi kuwa mnamo wiki mbili zijazo tayari club itarudi katika ubora mkubwa na muonekano mpya ikifuatiwa na maboresho ya upanuzi na samani zote za ndani zinazostahili katika kalbu za kijanja. Amezidi kuwaondoa shaka mashabiki wake kuwa hawatapoteza hata muda stahiki kuhakikisha burudani inarudi mapema sana akikiri kuwa club imebuniwa kiufundi zaidi.

IMEANDALIWA NA ALOYSON– 0755103054

Comments/ Maoni

Recommended for you